Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA),umesema umesikitishwa na kauli za baadhi ya viongozi wa dini zilizotolewa wakati wa baraza la Iddi za kuwataka warejee katika bunge maalum la katiba huku viongozi hao wakinyamaza bila ya kukemea matendo yaliyosababisha wajumbe wa umoja huo kususia vikao vya bunge hilo.
Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa umoja huo, Mwenyekiti wa chama
cha wananchi-CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, amesema UKAWA wanatambua kuwa
viongozi wa dini ni watu wenye heshima na nafasi ya pekee katika jamii,
hivyo wana kila sababu ya kuheshimu miito na ushauri wao.
Prof. Lipumba aliyasema hayo jana jijini Dar e s salaam wakati viongozi
wa UKAWA walipokutana kwa ajili ya kutoa tamko kuhusu miito ya viongozi
wa dini kuwataka kurejea kwenye bunge maalum la katiba Jumanne ijayo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo
CHADEMA Freeman Mbowe alisema kuwa anasikitika kuona kauli za viongozi
mbalimbali wa CCM pamoja na Serikali wakitoa matamko ambayo hayaashirii
kutafuta muafaka.
Aidha Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi Jemes Mbatia alisema ipo
haja ya serikali kuangalia namna ya kuboresha sheria ya uchaguzi ili
kutoa nafasi ya kufanyika kwa uchaguzi mwakani kutokana na dalili
zilizopo ni dhahiri kuwa katiba mpya haiwezi kupatikana katika kipindi
kilichopangwa.
UKAWA wamedai kuwa waliamua kuondoka bungeni ili kupinga njama
zilizokuwa zikifanywa na wajumbe wa chama cha Mapinduzi za kuhujumu
mchakato wa katiba mpya, kupinga kauli za kejeli, lugha za ubaguzi,
uchochezi na matusi, pamoja na kile walichosema ni kushindwa kwa
mwenyekiti wa Bunge hilo kuwadhibiti wajumbe wanaokiuka kanuni