SHIRIKA LA SUMASESU WILAYANI MAKETE LAIKABIDHI SEKONDARI YA LUPALILO VIFAA VYA MICHEZO

 Mkurugenzi wa shirika la SUMASESU Bw. Egnatio Mtawa(kulia) akimkabidhi jezi mkuu wa shule ya sekondari Lupalilo Mwl. Liombo.

Na Edwin Moshi, Makete.
Katika kuthamini umuhimu wa michezo katika shule mbalimbali, shirika la SUMASESU lililopo wilayani Makete mkoani Njombe limetoa vifaa vya michezo kwa shule ya sekondari Lupalilo iliyopo wilayani hapo. 

Vifaa vilivyotolewa ni mipira miwili ya miguu kwa wavulana, mipira miwili ya netiboli kwa wasichana pamoja na jezi 12 kwa wasichana. 

Akizungumza wakati wa kukabidhi jezi hizo, mkurugenzi wa SUMASESU Bw. Egnatio Mtawa amewataka wanafunzi hao kutumia muda wa mapumziko kwa ajili ya michezo ili kujenga kizazi cha wapenda michezo na mwishowe taifa lijivunie kuwa na wanamichezo wengi hasa waliojifunza kutoka shuleni. 

Amesema kutokana na michezo ya wasichana kutopewa kipaumbele kama ya wavulana ndio maana wamewapa mipira miwili pamoja na jezi ili nao washiriki kwa kasi katika michezo. 

"Leo sisi kama shirika tunawakabidhi zawadi hiazi za vifaa vya michezo, tunaomba mvitumie kuinua michezo katika shule hii na wilaya yetu kwa ujumla, kina dada wao tumewapendelea zaidi kwa kuwapa mipira na jezi na hii haimaanishi wao ni bora kuliko wavulana, hii ni njia mojawapo ya kuhamasisha michezo kwa wasichana ambao mara nyingi wamekuwa wakisahaulika" amesema Mtawa. 

Vifaa hivyo vimekabidhiwa kwa mkuu wa shule hiyo Bw. Johns Liombo mbele ya wanafunzi wote wa shule hiyo.

 Mwl. Fredrick Ndagala.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo mwalimu wa michezo shuleni hapo Mwl. Fredrick Ndagala amelishukuru shirika la SUMASESU kwa kutoa msaada huo na kusema kuwa itawsaidia kwa kiasi kikubwa kuinua michezo katika shule hiyo. 

Amesema kupatiwa msaada huo hakumaamishi kuwa SUMASESU wana uwezo mkubwa kuliko mashirika mengine ama wadau mbalimbali bali ni moyo wao wa kutoa huku akiwaomba wadau wengine kuisaidia shule hiyo kimichezo kwani bado wanahitaji msaada zaidi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo