Katika hali ya kuushangaza mtandao huu, mwandishi wetu katika pitapita zake amekuta hali ya uchafu (takataka) zikiwa zimetupwa katika mto unaopita nyuma ya majengo ya MTC Tandala wilayani Makete.
Miongoni mwa taka hizo ni pedi ambazo zimetumika, na haikufahamika mara moja kama taka hizo zimesombwa na maji ama zimetupwa na mtu
Jambo lingine la kusikitisha ni kwamba haifahamiki mara moja kama yanakoenda maji hayo yanatumika kunywa ama vipi. Hii ni hatari kwa afya za binadamu kama wanayatumia maji hayo kwa kunywa bila kuyachemsha, na hata yakichemshwa je uchafu huo na afya ya binadamu, mmmmmh.
Picha/habari Eddy Blog