MWANAMKE AVUA NGUO NA KUBAKI UCHI WA MNYAMA MBELE YA SANAMU YA NELSON MANDELA



Kisa cha mwanamke mmoja nchini Afrika Kusini aliyevua nguo zote na kubaki Uchi  kama  alivyozaliwa na kusimama mbele ya sanamu kubwa ya hayati Nelson Mandela, kimewaacha wapita njia na majirani waliokuwepo karibu na eneo hilo midomo wazi.

Kwa mujibu wa gazeti la Star, Jumatatu mchana ya wiki iliyopita mwanamke huyo ambaye hakufahamika alifika eneo la Sandton, Johannesburg ilipo sanamu hiyo akiwa amevaa vizuri. 
Ghafla akafanya kama ambavyo hufanya wakati wa kuoga, alitoa nguo zote na kusimama mbele ya sanamu hiyo na kuwapa watu onesho la bure huku wengine wakichukua picha na video exclusive za kupost katika mitandao ya kijamii.
 
Hata hivyo mwanamke huyo alipomaliza kufanya alichokuwa anakifanya (ambacho hakijulikani) alivaa nguo zake moja baada ya nyingine tena taratibu kama yuko chumbani kwake na kuondoka huku watu wakimshangaa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo