Siku mbili zilizopita kumekuwa na taarifa mitaani kuwa mwimbaji
ambaye pia ni producer wa Sharobaro Records, Bob Junior alifanyiwa fujo
na mwanaume mmoja anaedaiwa kuwa mume wa msichana aliyekuwa anafanya
naye video.
Taarifa hizo zilieleza kuwa tukio hilo lilifanyika maeneo ya Mlimani
City wakati Bob Junior alipokuwa akishuti vipande vya wimbo wake wa
‘Bolingo’ huku msichana huyo akijiachia mbele ya lens.
Ghafla mumewe akatokea na kuzua tafrani, video ya wimbo ikageuka kuwa
ya ndondi na mwisho wa siku mwimbaji huyo alilazimika kukimbia kupisha
shari.
Times Fm imeongea na Bob Junior kuhusu tetesi hizo ambapo
yeye amekiri kutokea kwa fujo hiyo lakini amekanusha kuhusu suala la
kufanya video na msichana huyo ingawa alikuwa na directors wake na
vifaa.
“Hapana, naona watu wanakuwa kama wambea. Mimi nilikuwa nimekaa pale
Mlimani City tunapiga story niko na mwanamke wangu. Rafiki yangu
mwingine alikuwa kakaa na mwanamke mwingine, sasa sijui kama ni mke wa
mtu au nini, ndio ikatokea vurugu lakini huyo mwanamke aliyefanyiwa
vurugu mimi simfahamu.” Ameeleza Bob Junior.
“Tulikuwa tumekaa tu tunaenjoy tunapiga story, tunakula…mimi sijui
kama ni mwanamke wake au ni mke wake. Amemfanyia vurugu, amemvuta
nywele. Wamezinguana kidogo lakini sifahamu kama ni mke wake au ni
mchumba wake ila najua ni mtu ambaye ana uhusiano nae.” Ameongeza.
Akizungumzia kuhusu taarifa kuwa alitoka nduki na kumuacha rafiki
yake akifanyiwa fujo, Bob ameeleza kuwa aliondoka kupisha shari na sio
kukimbia kama ilivyotafsiriwa.
“Hapana siwezi kukimbia siwezi kukimbia. Tanzania ni nchi yenye amani
kwa nini nikimbie kuna vita gani jamani hapo. Mimi nilichukua vitu
vyangu na vijana wangu na team Sharobaro wangu, nikaondoka taratibu
nikachukua gari langu nikaondoka. Unapoona mtafaruku hupaswi kukaa
kuendelea kuangalia jambo. Unapaswa kupisha uliache jambo liendelee.”