Kikongwe mwenye umri wa miaka 62 Raheli Jilungu mkazi wa kijiji cha
Mishepu katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga aliuawa kwa kukatwa shingo na mtuhumiwa
aliyetambulika kwa jina la Maganga Fuja akiwa na wenzake
watatu .Chanzo cha mauaji hayo ni imani potofu za kishirikina.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Justus
Kamugisha atoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Shinyanga kupambana na vitendo
vya mauaji ya vikongwe.
Kamugisha alisema kazi kubwa hivi sasa kwa
upande wake kuhakikisha mauaji yanakoma mkoani Shinyanga.alisema ufanisi
wa mapambano hayo yanategemea ushirikiano kutoka kwa wakazi wa mkoa
wake kwa kutoa taarifa za wausika wa mauaji hayo.
alisema mauaji hayo
yamekuwa na mtandao mkubwa wakiwemo ndugu wa marehemu wanaofanyiwa
vitendo hivyo.
Pia kuanzia Januari mpaka desemba mwaka 2013 mkoa ulikuwa na mauaji
ya vikongwe 27 huku watuhumiwa 16 wakifikishwa mahakamani na kuanzia
mwezi Januari hadi Julai mwaka huu vikongwe 11 wameuwawa huku
watuhumiwa 16 pia wakifikishwa mahakamani.