Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) Mbeya mjiji John
Mwambigija “Mzee wa Upako” akiwahutubia wananchi wa Kata ya Manga jiji Mbeya,
wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo hilo Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ katika zira ya
kutoa taarifa ya utekeleza wa ahadi alizo toa mwaka 2010 wakati akiomba ridhaa
ya kuwa Mbunge (Picha na Kenneth Ngelesi)
Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi akiwa hutubia wananchi wa
Mtaa wa Mafiat kata ya Manga jiji Mbeya katika Mkutano wa hadara ambo ni kwa
ajili ya kuto taafifa za utekelezaji wa ahadi alizotoa mwaka 2010 wakati akiomba ridhaa ya kuwa
Mbunge
NA KENNETH NGELESI,MBEYA
SIKU
chache baada ya kupata viongozi wapya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema),Mkoani hapa kimesema kimejipanga kufanya mikutano kila kata kwa ajili
ya kutoa elimu ya Uchuguzi wa Serikali za mitaa unao tarajia kufanbyika Oktoba
Mwaka huu.
Chama hicho kimekusudia kumbana na
chama cha Mapinduzi ili kujihakikishia ushindi wa kishindo na kuweza kukibura chama cha Mapinduzi CCM
katika uchaguzi huyo.
Akiwahutubia wananchi jana na
Mwenyekiti wa chama hicho, Wilaya ya Mbeya Mjini, John Mwambigija, katika
mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Nsalala, Mjini Mbalizi,alisema
kuwa mikutano hiyo itakayofanyika kila kata na kwamba imepewa jina la bandika bandua.
Mwenyekiti huyo ambaye ametetea
nafai hiyo katika uchaguzi ulio fanyika Agost mwaka huu alisema chama hicho,
mkoa wa Mbeya licha ya kutumia mikutano hiyo kuwajengea uwezo wananchi kabla
hawajafikia hatua ya kufanya maamuzi ya kuwachagua viongozi wao wa serikali za
mitaa katika uchaguzi wa Oktoba, lakini pia inalenga kukiimarisha chama hicho ngazi
za chini.
Mwambigija alisema wananchi katika
ngazi za mitaa, vitongoji na kata wanafursa ya kujua umuhimu wa kuchagua
viongozi bora, wataoweza kuwawezesha kupata maendeleo wanayoyatarajia badala ya
kuendelea kulalamika.
Katika mkutano huo uliokusanya mamia
ya wananchi wa kata hiyo ya Nsalala, jumla ya wanachama 15 kutoka Chama cha
Mapinduzi (CCM) walirudisha kadi na kukabidhiwa kadi mpya za chadema.
Wakati wanachama hao 15 wakirudisha
fomu za CCM, chama hicho cha Chadema kilifanikiwa kuvuna wanachama wapya 71 waliochukua
fomu na kula kiapo cha kuwa wanachama.
Viongozi mbalimbali wa Chadema,
akiwemo Mbunge wa jimbo la Mbeya, Mjini Joseph Mbilinyi (Sugu), ambaye na
ameungana na wenzake wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kugomea bunge la
katiba , ameungana na viongozi wake wa mkoa kuendesha mikutano hiyo ya bandika
bandua katika kata mbalimbali mkoani Mbeya.