Waziri mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda ameziagiza halmashauri za wilaya
nchini kuendelea na matayarisho ya uchagauzi mkuu wa serikali za mitaa
unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu huku jitihada zikifanywa
na serikali kuwaomba umoja wa katiba ya wananchi -UKAWA kukubali
kuridhia ombi la kurudi bungeni ili azma hiyo iweze kufikiwa.
Mheshimiwa Pinda ametoa agizo hilo wakati
akizungumza na wakurugenzi, wenyeviti na viongozi wa serikali ngazi ya
taifa katika kikao cha pamoja kilichofanyika jijini Tanga.
Amesema kama kutakuwa na mabadiliko kuhusu
kuahirishwa kwa uchaguzi huo huku pande zote mbili zikirudi kuendelea na
bunge la katiba viongozi hao watapewa taarifa kuhusu mchakato huo
lakini matayarisho ya uchaguzi mkuu wa serikali za mitaa ni lazima
yafanyike.
Kuhusu uwekezaji waziri mkuu ameziagiza halmashauri
za wilaya nchini kuhakikisha kuwa wanatangaza fursa za uwekezaji
zilizopo katika maeneo yao kama walivyofanya mkoa wa Tanga mwishoni mwa
mwaka jana ambapo walifanya kongamano la uwekezaji lililoshirikisha
wawekezaji wa ndani na nje ya nchi hatua ambayo imeanza kuleta mafanikio
kwa Tanga na taifa kwa ujumla .
>>Tazama video hapo chini kumsikiliza.
>>Tazama video hapo chini kumsikiliza.