Hapa
ni katika eneo la dharura katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga ambapo
majeruhi 29 hadi sasa wamepokelewa kufuatia ajali ya gari aina ya fuso
iliyokuwa imebeba watu wengi pamoja na mizigo kuelekea katika mnada wa
Mhunze uliopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.
Ajali hiyo imetokea
asubuhi ya leo Alhamis.Pichani majeruhi waliendelea kuhudumiwa na
wataalam wa afya katika hospotali ya mkoa wa Shinyanga
 |
Kwa
mujibu wa kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt
Maguja Daniel ameiambia malunde1 blog kuwa mpaka sasa wamepokea miili
miwili ya marehemu na majeruhi 29 |
 |
Huduma inaendelea kutolewa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga |
 |
Baadhi
ya majeruhi wameiambia malunde1 blog kuwa gari aina ya fuso waliyokuwa
wamepanda tena kwa kujazana ilikuwa inafukuzana na fuso nyingine na
ghafla walijikuta wakiwa wameshapinduka |
 |
Kulia ni kaimu
mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Maguja Daniel
akichukua maelezo kutoka kwa askari wa usalama barabarani |
 |
Majeruhi akipelekwa wodini |
 |
Miili ya marehemu ikiwa katika eneo la dharura katika hospitali ya mkoa wa shinyanga |
 |
Kaimu
mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Maguja Daniel
akizungumza na waandishi wa habari hivi punde-Picha zote na Kadama
Malunde-Malunde1 blog
|
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi