RAIS KAGAME ASEMA TANZANIA NA RWANDA NI NDUGU NA WATAENDELEA KUWA NDUGU



Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema kwamba Rwanda na Tanzania ni mataifa ndugu na yataendelea kuwa ndugu kwa sababu yanachangia undugu huo. 

Rais Paul Kagame ameyasema hayo mjini Kigali kwenye kikao na waandishi wa habari.

Hata hivyo ameonya kwamba Rwanda itapambana na yoyote anayeshirikiana na FDRL. Amesema dunia hii ni ya ajabu maana inawasikiliza na kuwatunza wauaji halafu inalazimisha maridhiano.

"Inawezekana tuna sauti ndogo, hatusikiki lakini nawaakikishia hatutaridhiana na wauaji zaidi ya kupambana nao na marafiki zao" alisema.
 
Nchi za Rwanda na Tanzania zilikabiliwa na wakati mgumu kuanzia mwaka jana kutokana na kutofautiana kuhusu kundi la waasi wa kihutu la FDLR linaloendesha mambo yake mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo dhidi ya utawala mjini Kigali.
 
Mwandishi wetu Sylivanus Kalemera kutoka Kigali ana ripoti zaidi. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo