Jumla ya maboks miatano sitini na nane yamekamatwa na jeshi la polisi
Kagera yakiwa na vipodozi haramu pamoja na dawa za binadamu.
Akiongea mkoani Kagera kamanda wa jeshi la polisi wa mkoa huo Henri
Mwaibambya amesema vipodozi hivyo vilikamatwa katika tarafa ya bugabo
wilayani Bukoba vikiwa ndani ya ziwa victoria vikiwa vimeingizwa nchini
kutoka nchi jirani ya Uganda kwa njia ya magendo huku vikiwa
vimepakiwa ndani ya mtumbwi wa mbao wenye namba za usajili TMZ 010078,
ambapo amewataja watuhumiwa walio kamatwa kuwa ni Otanga Jaluo-miaka 34
mkazi wa Pasiasi Mwanza, Yusuph Juma-miaka 46 mkazi wa Mwanza na Eleven
Sylivester Msimbiti -miaka 43 mkazi wa Mwanza.
Aidha kamanda huyo wa jeshi la polisi amethibisha kutokea kwa kifo
cha mauaji ya mtoto mchanga mwenye umri wa miezi tisa aitwae Angel
Abeid, ambae ameuawa usiku wa kuamkia leo na mama yake mzazi Vaileth
Kalumuna-miaka18, ambapo ameongeza kuwa mama huyo alimbana pua na mdomo
wa mtoto huyo hadi akapoteza maisha, na baada ya kuhojiwa na jeshi la
polisi mama huyo alieleza chanzo cha kumuua manae kuwa ni ugumu wa
maisha.