Diamond Platinumz ametangaza kupitia Instagram kuwa ataachia video mbili kwa mpigo ikiwa ni siku chache baada ya kumalizana na BET Awards 2014.
Mashabiki wake wategemee kuona video mbili kwa wakati mmoja ambazo ni
moja ya wimbo aliofanya na mkali wa Kukere, Iyanya wa Nigeria, na
nyingine ya wimbo wenye asili ya ngoma za kitanzania Kitorondo aliyoipa
jina la MdogoMdogo.
Diamond ameendelea kushare picha mbalimbali kutoka kwenye video hizo,
picha zinazoashiria kuwa video hizo zitakuwa tofauti kabisa na video za
awali za Diamond.
Katika moja ya picha alizoshare Instagram akiwa katika eneo lenye
miamba na maporomoko ya maji huku akiwa amevaa kama mtu anaeishi
nyikani, aliwataka mashabiki wataje uhusika wake.