Mwili wa Sista baada ya kupigwa risasi.
Majambazi watatu wamemuua kwa kumpiga risasi kichwani Mhasibu wa Kanisa Katoliki, Usharika wa Makoka, jijini Dar es Salaam, Sista Prisencia Kapuli na kisha kumpora fedha zinazokadiriwa kuwa zaidi ya Sh milioni 10 alizokuwa nazo.
Tukio hilo ni la jana saa 9 alasiri katika eneo la Ubungo Riverside wakati Prisencia, mtawa mwenzake pamoja na dereva wao, Mark Mwarabu, walipokwenda katika eneo hilo kununua mahitaji.

Sista Kapuli
ameuwawa kwa kupigwa risasi kichwani na majambazi hayo baada ya kufuatiliwa nyendo zao wakitokea katika benki ya CRDB
ambayo tawi lake halikufahamika mara moja wakati akimsubiri Sista Mwenzie
aliyeshuka katika gari walilokuwa wamepanda lenye namba za usajili T
213 CJZ Toyota VX kwa ajili ya kwenda kuulizia bidhaa fulani dukani
katika eneo hilo la Riverside Ubungo jijini Dar es Salaam.
Gari lenye namba za usajili T 213 CJZ alilokuja nalo marehemu.
Akisimulia tukio hilo dereva wa gari la masister hao Bw Marck Patrick Mwarabu amesema kuwa majambazi hayo yalikuwa matatu na alipojaribu kuyadhibiti kwa kufunga mlango wa gari walimjeruhi vibaya kwa risasi katika dole gumba lake na kisha kutoweka na pochi ya marehemu Kapuli kwa kutumia usafiri wa pikipiki.

Mmoja wa waendesha Bajaji Bw Godfrey Severine
ambaye amenusurika katika tukio hilo bada ya Bajaji yake kupigwa risasi
kadhaa amesema kuwa watu hao walifyatua risasi kadhaa zilizosababisha
taharuki kwa wananchi ambao walikuwa wakikimbia hovyo na hivyo kupata
upenyo wa kutoweka katika eneo hilo.
Dereva akisimulia tukio zima la yeye kupigwa risasi na sista aliyekuwa naye kuuawa.
Diwani wa kata ya Makuburi Bw William Mfungo aliyeshuhudia pia tukio hilo amesema wakati umefika sasa kwa jeshi la polisi kujizatiti kudhibiti matukio hayo kutokana na majambazi kutumia silaha nzito ambazo wananchi hawawezi kupambana nao na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pale wanapobaini njama kabla ya tukio kutokea.

Jeshi la polisi wakiwa na silaha walifika katika
eneo la tukio na kuondoka na mwili wa marehemi licha ya kukuta majambazi
hayo yameshatoweka katika eneo la tukio.
Mwili wa Sista Kapuli ukipakizwa ndani ya gari la Polisi
Diwani wa kata ya Makuburi Bw William Mfungo akizungumzia tukio hilo.