
Wanafunzi
wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wanaolipiwa na Bodi ya Mikopo
wakimsikiliza Makamu Mkuu wa Chuo hicho aliyekuwa akiongea nao.
Makamu Mkuu wa Chuo akijaribu kuwatuliza wanachuo hao kwa kuwaahidi kushughulikia suala lao.
Viti vikiwa vimetawanywa baada ya vurugu zilizosababishwa na mgomo huo.
WANAFUNZI wanaolipiwa na Bodi ya Mikopo katika Chuo cha Taifa cha
Usafirishaji (NIT) kilichopo Mabibo Mwisho jijini Dar, leo wamegoma na
kufanya vurugu wakidai
kucheleweshewa fedha zao za mkopo.
Mgomo huo
umeanza majira ya saa 6 na nusu mchana ambapo polisi waliingilia kati
kutuliza ghasia zilizokuwa zinaendelea chuoni hapo. Mpaka mtoa habari
hii anaondoka eneo la tukio, bado wanachuo walikuwa wakisubiri majibu ya
uongozi wa chuo hicho.
CREDITS:GPL
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi