SERIKALI imewapa uraia wa Tanzania
Wakimbizi wa Kisomali wenye asili ya Kibantu 1,514 waliokuwa wanaishi
katika Makazi ya Chogo, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Wakimbizi hao ambao walikimbia nchi
yao Somalia baada ya vita kutokea mwaka 1990 ambapo baadhi yao 3,000
walikimbilia nchini kwa kutambua kuwa ndipo mababu zao walikotoka,
Serikali iliwapokea na kuwahifadhi katika Kambi ya Mkuyu iliyopo Mkoani
Tanga ambapo walikuwa wakipata msaada kutoka Shirika la Kuhudumia
Wakimbizi Duniani (UNHCR).
Akizungumza jana baada ya kuwapa vyeti
vya uraia wakimbizi hao ambao kwasasa ni raia halali wa Tanzania,
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe alisema wakimbizi hao
walihamishwa na Serikali mwaka 2003 kutoka Kambi ya Mkuyu kuja katika
Makazi ya Chogo ili wapatiwe mashamba kwa ajili ya kujishughulisha na
kilimo ili waweze kujitegemea.
"Nachukua nafasi hii kuwapongeza wote
waliopewa uraia wa Tanzania, wajisikie kuwa wao ni raia huru sawa na
Watanzania wengine. Hata hivyo nawasihi muwe waadilifu na watiifu kwa
sheria zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania," alisema Chikawe.
Chikawe pia alitoa pongezi kwa UNHCR kwa kujenga miundombinu muhimu katika makazi hayo ya Chogo na pia kuwawezesha wakimbizi hao kuishi maisha ya kujitegemea wenyewe kabla hata ya kuwa raia.
Hata hivyo, Waziri Chikawe aliwataka wakimbizi 150 katika makazi hayo ya Chogo ambao hawakuomba kuwa raia wa Tanzania kwa nia ya kurudi nchini Somalia pale hali ya amani itakapopatikana wanapaswa kuendelea kutii sheria za nchi zinazotawala hifadhi ya ukimbizi nchini.
Aidha, Mwakilishi Mkazi wa UNHCR, Joyce Mends-Cole katika hafla hiyo aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwapa uraia wakimbizi hao na Shirika lake litaendelea kutoa misaada mbalimbali kwa wakimbizi waliobaki katika makazi hayo pamoja na sehemu nyingine nchini.
Hafla hiyo ya ugawaji wa vyeti vya uraia ilihudhuriwa na Maofisa wa Idara ya Wakimbizi na Uhamiaji zilizopo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwakilishi wa Mkuuu wa Mkoa wa Tanga na Serikali ya Kijiji cha Chogo pamoja na Maofisa wa UNHCR.