Magari mawili aina ya Coaster
yanayosafririsha abiria kati ya Mwenge, Tegeta na Mbezi jiijini Dar,
yamegongana na kuua abiria wanaokadiriwa kufikia zaidi ya 10.
Ajali
hiyo imetokea mchana JANA eneo la Makongo. Mashahuda wa ajali hiyo
wamesema kuwa uzembe uliofanywa na dereva wa daladala iliyokuwa ikitoka
Tegeta ndio uliosababisha ajali hiyo kwani alipita upande usio wake.






