Mzee wa kanisa la kiroho (jina linahifadhiwa kwa sasa), aliyetajwa
kwa jina la Luca Pesa, mkazi wa Segerea, Dar, ameaibika baada ya
kukurupushwa kwenye nyumba ya kulala wageni (gesti) akidaiwa kutaka
kuvunja amri ya sita na binti ambaye ni msanii chipukizi wa filamu za
Kibongo, Debora Jacob.
Tukio hilo ambalo kamwe Luca hawezi kulisahahu
maishani mwake, lilijiri kwenye gesti hiyo iliyopo karibu na Kituo Kikuu
cha Mabasi cha Segerea, Dar, Jumanne iliyopita huku mzee huyo
akishushiwa tuhuma nzito ya rushwa ya ngono kwa vibinti chini ya miaka
18.
Katika tukio hilo, mzee huyo wa kanisa na msanii huyo wa Kundi la
Maigizo la Vivif lenye maskani yake maeneo hayo walikuwa wamejichimbia
kwenye gesti hiyo katika chumba ambacho mlangoni kilikuwa kimeandikwa
Rombo kabla ya kuchomolewa na kufikishwa kanisani kisha polisi.
Fumanizi
hilo lilikuwa limesukwa na wasanii wa kundi hilo kwa lengo la
kumkomoa mzee huyo wa kanisa ambaye alikuwa ni mfadhili wa kundi
lao aliyeanza kutumia mgongo wa ufadhili kuwatongoza mabinti
wa kundi hilo mmoja baada ya mwingine.
Wakiwa ndani ya gesti hiyo, wasanii wa kundi hilo walivamia chumba hicho na kuanza kumchomoa mzee huyo ambaye aliruka ukuta
na kudondokea kwenye matuta ya viazi.
Akiwa anajizoazoa kwenye matuta hayo, kundi la wasanii hao
lilimuunganishia ambapo kabla ya kumnasa aliingia kwenye chumba cha
nyumba iliyopo jirani na gesti hiyo ili kujisalimisha.
Hata hivyo,
zoezi lake lilifeli baada ya wasanii hao kumtahadhalisha mwenye nyumba
hiyo kuwa wanamtaka mtuhumiwa wao la sivyo wangeichoma moto.
Baada ya kuzingirwa na wasanii hao huku akihatarisha maisha yake kwa
kuwa wasanii hao walikuwa na hasira, aliona yasiwe makuu akaamua
kuwaruhusu wamtoe mtuhumiwa wao wakamalizane naye kanisani.
Alipotiwa mikononi, mzee huyo wa kanisa aliomba apelekwe
kanisani ambapo hapakuwa mbali na eneo la tukio ili akahifadhi vitu
vyake muhimu pamoja na kuomba ushauri.
Kundi hilo la wasanii lilimpeleka
kanisani msobemsobe ambapo baada ya hatua kadhaa polisi walitokea na
kuwadhibiti wananchi wenye hasira na wasanii waliotaka kumdhuru mzee
huyo wa kanisa wakati akipelekwa kanisani.
Wakiwa mitaani, njiani mabinti walikuwa wakipiga
kelele ‘weraaa…ukomeee…’ huku wakifurahia kufunga mitaa kwa madai kwamba
mzee huyo wa kanisa alizidi.
Katika sekeseke hilo, polisi hao walimtia pingu mzee huyo wa kanisa na kuongoza safari ya kuelekea kanisani.
Wakiwa kanisani hapo polisi walijitambulisha na kuwauliza wachungaji
pamoja na waumini wa kanisa hilo kama walimfahamu mzee huyo wa kanisa.
Kundi la wazee pamoja na vijana wa kanisa
hilo walikiri kuwa Luca ni mmoja wa wazee wa kanisa hilo ndipo polisi
hao wakamruhusu kuwakabidhi baadhi ya vitu vyake ikiwemo simu na fedha
kisha breki ya kwanza ikawa Kituo cha Polisi cha Tabata-Shule ambapo
alifunguliwa jalada la kesi namba RB/3843/2014 -RUSHWA YA NGONO,
KUWAWEKA KAMBI KINYUME CHA SHERIA WASICHANA WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 18
NA KUWADHALILISHA KIJINSIA.
Chanzo: Ijumaa/ Gpl
Chanzo: Ijumaa/ Gpl