skip to main |
skip to sidebar
MTANGAZAJI MAARUFU SSEBO AJIUNGA RASMI REDIO E FM
Mtangazaji maarufu nchini wa vipindi vya Radio na Television
Dennis Busulwa a.k.a Ssebo amejiunga na Radio ya E FM ambayo
imekwishajizolea umaarufu mkubwa jijini Dsm kwa kipindi kifupi tu
kutokana na staili yake tofauti ya urushaji matangazo nchini.
Ssebo
mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka mitano kwenye vituo mbalimbali vya
Radio na TV amejizolea sifa na mashabiki lukuki katika tasnia hii ya
utangazaji kutokana na staili na vituko vyake awapo hewani.
"Mashabiki
wangu watarajie mengi mazuri kutoka kwangu nikiwa na E FM",alisema
Ssebo.Ssebo anakutana na timu ya watangazaji wengine wakongwe kama Dj
Majey, Dizzo One na Sos B waliokwisha anza kusikika Radioni hapo.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi