MSICHANA ALIYEPIGWA NA CHID BENZI AONDOKA NCHINI

MSICHANA aliyewahi kupigwa na msanii wa Hip Hop Bongo, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’, Mwanaisha Sued ‘Aisha’ ametimkia nchini Afrika Kusini kuishi kwa muda.

Paparazi wetu alitia timu nyumbani kwa binti huyo Ilala-Bungoni, jijini Dar ili kujua maendeleo yake ambapo mdogo wa Asha ambaye hakutaka jina lake lichorwe gazetini, alijibu kwa kifupi:

“Aisha hayupo amekwenda Sauzi kwa muda, kuhusu alichokifuata mimi sijui. Ila hajambo na anaendelea vizuri.”

Aprili mwaka huu, Chid Benz alishtakiwa katika kituo cha Polisi cha Pangani, Ilala kwa kosa la kumshambulia Aisha ambaye aliwahi kuwa mpenzi wake.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo