Mke
halali wa Rais wa bendi ya mashujaa musica Charles Gabriel
Cyprian 'Chaz Baba', Rehema Sospeter Marwa mwishoni mwa wiki
jana alizua timbwili la mwaka baada ya kumchapa makofi msichana
mmoja ajulikanaye kwa jina la Husna....
Tukio
hilo lililoshuhudiwa na mwandishi wetu lilitokea majira ya saa
nane za usiku katika ukumbi wa Letas ( zamani Busness Park)
uliopo Makumbusho wakati bendi ya Mashujaa ilipokuwa inatoa
burudani.....
Sakata
zima lilikuwa hivi;Husna alikuwa anakunywa kwenye Pub hiyo,
mara akatokea mke wa Chaz Baba na kumfuata kaunta Husna na
kumwambia amependeza sana kwa pamba alizotupia kisha akamuomba
amsindikize chooni....
Wakati
wanaongea, mwandishi wetu aliwasikiliza na kuanza kuwafuatilia
hadi chooni. Walipofika chooni Rehema alimkunja Husna na
kumwambia kuwa yeye ni mke halali wa Chaz Baba hivyo
anamuomba aachane na mume wake lasivyo atamng'oa meno....
"Sikia
nikwambie wewe binti, mimi ndo mke halali wa Chaz Baba, hivyo
nakuomba kiustaarabu uachane na mume wangu lasivyo utahama
mjini bila kupenda, " alisikikia akisema Rehema huku akiwa amemkwida Husna.
Hata
hivyo Husna alijitetea kwamba hana mahusiano na Chaz Baba
kwani walishaachana muda mrefu na kumtaka Rehema asikurupuke....
"Nisikilize
wewe mwanamke, siku nyingine usiwe unakurupuka kama kichaa,
kuolewa unajiona umefika ee!! Sasa kwa taarifa yako huyo Chaz
baba nilishamtema kitambo tu, achana na mimi, hangaika na
wengine.....Kwanza jichunge wewe mwanamke," alisikika akisema Husna.
Kauli
hiyo ilimkera Rehema na kumtia Nakozi mbili za moto ( makofi
mawili adimu) Husna aliyekuwa amevalia kigauni cha rangi
nyekundu kisha akaondoka na kurudi kupata kilaji ndani ya Pub
hiyo wakati mumewe akiendelea kutumbuiza....
Baada
ya tukio hilo, mwandishi wetu alimfuata Rehema ambaye alikuwa
na wapambe wa kutosha na kumuhoji kulikoni kupigana
chooni..!!!!??
"Ndo ivo, nshamtandika vibao, nilikuwa nampa onyo aachane na mume wangu, ni hilo tu," alijibu Rehema.
Husna aliporudi ukumbini alianza kuelezea tukio zima lilivyokuwa hadi kuchapwa makofi,
"Mimi namshangaa sana yule mwanamke, yaani kiukweli Chaz Baba
nshafanya naye mapenzi siku nyingi na nimeshaachana naye. Sasa
namshangaa anakuja kuniuliza leo na kunipiga chooni, ila we
acha tuu, kuna kitu ntamfanyia, asidhani namwogopa,"alisema Husna.
