June 05 2014 mchana kupitia mitandao mbalimbali Tanzania zilisambaa taarifa zikimuhusu mmiliki wa mojawapo ya nyumba maeneo ya Sakina jijini Arusha kwamba nyoka aliyekua akimfuga kwa siku nyingi na kuhusishwa na imani za kishirikina, ameuwawa na Wananchi.
Wananchi
walimuua nyoka huyo na kisha kumkata kata vipandevipande ambapo baada
ya hizi taarifa kusambaa mmiliki wa nyumba hii ameamua kufunguka ili kutoa maelezo yake ambayo anadai ndio ukweli wenyewe.
Mr.Joseph Paschal Magesa anasema, "Mimi kama mimi kwanza ni
Mkristo safi na mzee wa kanisa na niliondoka nyumbani jana na mke wangu
kutoka Arusha kuelekea Dar es salaam, sijui lolote kuhusiana na hicho
kitu ila nilipofika maeneo ya Mwanga na Same nikapigiwa simu kwamba kuna
nyoka huku ndani ya eneo la garden nyumbani, kuna vijana niliwaacha
wawili pale nyumbani nikawaambia waambieni watu wawasaidie kumuua huyo
nyoka"
"Wakamuita jirani yangu hapo ndipo naye akanipigia simu nikamwambia
bwana wewe si una bunduki nisaidie kumuua huyo nyoka ila alivyokata simu
nilijua ametekeleza kumbe aliondoka, baadaye napiga tena simu nauliza
vipi naambiwa bado yupo na watu wamejaa nikawauliza kwani hao watu
hawawezi kumuua mpaka bunduki wakasema wanaweza ndio baadae wakanambia
wamemvuta mkia wamemuweka nje ya geti"
"Nikawauliza
anavutika, asije akawa analeta shida wakasema anavutika, nikawaambia
mpelekeni kanisani kwa sababu nyumbani kwangu ni jirani na kanisa ndio
wakamvuta hadi kanisani wakammwagia maji ya baraka kisha wakamkatakata
ndo ikawa mwisho wake hapo".
"Kusema kwamba nilikua nafuga kwamba huyu nyoka ni mtoto wangu wa
kwanza….. sasa kama ni mtoto wangu wa kwanza si inamaana na mtoto wangu
angekufa na yeye? mimi nasema namwachia Mungu tu…….. sijawahi kusikia
Nyoka kuishi maeneo hayo toka nimeanza kuishi kwa karibu miaka 8, hata
na mimi inanitatiza manake nimetumiwa picha Nyoka amefungwa kitambaa
chenye maandishi mekundu kama ya kiarabuarabu hivi….."
"Taarifa
kwamba Nyoka huyu amevunja kioo cha dirisha akiwa anatokea ndani ya
nyumba, sio kweli…. haipo kabisa hiyo kitu eti kwamba ametokea ndani,
hayo ni mambo ya watu tu… hicho kioo nilikivunja mimi wakati napanga
mizigo ya ofisi yangu… sifahamu chochote kuhusu huyu Nyoka, Watanzania
waniamini haya ninayosema ndio yanayotoka moyoni mwangu"

