 |
Hali ilivyokuwa katika mgomo huo abiria wakiwa wamejaa stendi ya mabasi Kahama bila kujua hatma yao |
Jeshi
la Polisi kitengo cha usalama barabarani Wilayani Kahama mkoani
Shinyanga limefanikiwa kuzuia mgomo wa madereva wa mabasi yaendayo
mikoani ambao wanapinga kutozwa faini isiyohalali na Kufanyiwa
udhalilishaji na baadhi ya Askari wa kitengo hicho.
Mabasi
yanayosafirisha Abiria Kutoka kahama kwenda mikoani leo yamegoma
kusafirisha abiria wakishinikiza serikali kuingilia kati suala la
faini wanazotozwa na askari wa jeshi la polisi kitengo cha usalama
Barabarani.
kwa mujibu wa farajimfinanga.com ni kuwa
imefika eneo la kituo kikuu cha mabasi mjini Kahama majira ya saa 12.30
asubuhi na kukuta mgomo huo ukiendela huku madereva wakiwa hawapo
katika mabasi yao hali iliyosababisha kuwepo kwa msongamano.
 |
Kaimu
mkuu wa kitengo cha usalama Barabarani Wilayani kahama Thomas Myonga
akiwa na maafisa wengine wa kikosi cha usalama barabarani pamoja na
waandishi wa Habari |
Kwa
mujibu wa Madereva ambao hawakutaka kutaja majina yao wamedai, wamekuwa
wakipigwa faini na askari wa mkoa wa Singida na huwalazimisha kulipa
faini kubwa ya zaidi ya Shilingi 200,000 huku stakabadhi ikiandikwa
shilingi 30,000 inayotambulika serikalini.
Wamesema pia
wamekuwa wakilazimishwa kupigwa picha mbele ya mabasi yao wanapokamatwa
hata kama wanaendesha mwendo mdogo na kwamba hubambikiziwa kesi, na baadhi ya madereva wamefikishwa mahakamani kwa kubambikiziwa
makosa pale wanapogoma kutoa faini.
Aidha wanapinga kitendo cha
ukatili alichofanyiwa dereva Mwenzao wa basi la Princess Munaa Lenye
No. T 183 CRW ambaye alivunjwa mkono na askari wa kitengo hicho huko
Mbezi Jijini Dar es Salaam baada ya kugoma kunyang’anywa leseni yake.
Hata
hivyo mgomo huo ulioanza saa kumi na mbili Asubuhi umedumu kwa
takribani saa mbili na baadaye kuanza kwa safari, huku ikielezwa kwamba
mgomo huo ulikuwa ni siri ya Madereva kwani Mawakala wanaokata tiketi
hawakuwa na taarifa.
Akizungumza wakati wa mgomo huo Kaimu
mkuu wa kitengo cha usalama Barabarani Wilayani kahama Thomas Myonga
aliwataka madereva kuendelea na safari zao kwani mgomo huo ni batili na
wanaweza kuzisababishia kapuni zao hasara kubwa endapo abiria
watafungua Mashitaka mahakamani.
Amewataka madereva kufuata
sheria za kudai haki zao ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa sehemu
zinazohusika ili masula yao yashughulikiwe pasipo kuleta athari
yoyote.
Mgomo huo wa madereva wa mabasi umefanyika katika Miji
ya Kahama, Bukoba, Mwanza, Msoma na Dar es Salaam huku taarifa zikisema
licha ya mgomo huo kumalizika ila kwa sasa maderewa wanaendesha kwa
mwendo wa chini kupita kiasi na kwa msongamano, hali inayozidi
kuwachelewesha abiria.
 |
Askari polisi wakiangalia hali ya usalama wa abiria kufuatia mgomo huo |
 |
Abiria wakiendelea kutawanyika huku mgomo ukiendelea |
 |
Abiria wakiwa bado katika hali ya Taharuki |
 |
Mgomo ukiendelea |
 |
Afande Toma akizungumza na abiria pamoja na Madereva mara baada ya suluhu ya mgomo kupatikana |
 |
Mabasi yakianza kuelekezwa kutoka stand na kuanza safari |
 |
Mabasi yakiendelea kuondoka kuelekea mikoani |
 |
Mabasi yakiendelea kuondoka kuelekea mikoani |
 |
Mabasi yakiendelea kuondoka kuelekea mikoani |
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi