KIJANA ANUSURIKA KUUAWA KWA KIPIGO BAADA YA KUTUHUMIWA KUIBA, LAKINI BAADAYE IKABAINIKA SI MWIZI



Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina moja la sule amenusurika kifo baada ya kupigwa na watu wenye hasira kali wakimtuhumu kuwa ni mwizi jambo ambalo baadaye lilikuja kubainika kuwa hana hatia yoyote. 
 
Wakizungumza eneo la feri jijini Dar es salaam baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa inasikitisha kuona watu wakijichukulia sheria mikononi bila kuhoji tukio ambapo mara baada ya kipigo ambacho kimemsababishia majeraha makubwa kijana huyo hakuna mtu aliyejitokeza kulalamika kuibiwa wala kujulikana kijana huyo ameiba nini.
Akiongea kwa shida kijana huyo amesema kuwa yeye hakuiba chocho na hajui kwa nini watu walimvamia na kuanza kumpiga
 
Katika hatua nyingine ya kujaribu kunusuru maisha ya kijana huyo baadhi ya wasamalia wema waliamua kumfikisha kijana huyo katika vyombo vya usalama lakini mara baada ya kumfikisha katika kituo kidogo kilichopo karibu na hapo walikuta kituo hicho kimefungwa na kufuri na hakuna askali yoyote lakina baada ya muda askali polisi mmoja alitokea..

Bonyeza  hapo  chini  kuona  video  ya  tukio  hilo
CHANZO:ITV


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo