Mrembo Millen Magese amekumbuka kauli ya kwamba mipango si matumzi, kutokana na kuwa na mipango mingi na marehemu Kanumba enzi za uhai wake katika kuikomboa sanaa ya filamu nchini, lakini kabla hawajakutana naye mauti yalimkuta...
Millen
na muigizaji mashuhuri nchini Nigeria, Ramsey Noah walipanga
kukutana na Kanumba lakini kabla siku hiyo haijafika kifo
kilimkuta Kanumba na mipango yote ikaharibika....
Millen
alifafanua hayo katika mahojiano maalumu na Mwandishi wetu
wakati akitangaza kampeni yake ya kuhamasiaha wanawake
wanaosumbuliwa na maumivu ya tumbo yasiyo ya kawaida pindi
wanapokuwa katika mzunguko wa hedhi zao ambapo kitaalam
hujulikana kama Endometriosis ambapo amegundua kwamba kati ya
wanawake 100 wa Tanzania, wanawake 12 hadi 15 wanasumbuliwa na
tatizo hilo...
Akikumbuka
siku ya kifo cha Kanumba kabla hawajakutana na kuzungumzia
masuala mbalimbali kuhusiana na filamu za Tanzania na namna ya
kupiga hatua nyingine mbele,Millen alisema:
"Iliniuma
sana kipindi kile maana nilikuwa nipo nchini na tulipanga
mimi, Kanumba na Noah lakini ndio ikawa hivyo lakini kwa
filamu zetu bado tunatakiwa kusoma zaidi ili tujue mambo mengi
na pia tutengeneze wigo mpana wa marafiki kutoka nje kama
mimi kwa sasa nina marafiki wengi akiwemo Ramsey Noah, Genevieve
Nnaji, Albal na wengine wa Marekani"
Katika
kusaidia tasnia hiyo, mrembo huyo anayemhusudu mrembo na
mwanamitindo Tausi Likokola,Iman,Flavian Matata, na Harieth Paul
alisema mwelekeo wake baada ya kukamilisha masomo yake ya
uigizaji, ataandaa filamu yake binafsi itakayoelezea maisha yake
halisi na tatizo linalomkabili na pia ataandika hadithi
kuhusiana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, Albino.
"Kwa
sasa nasomea namna ya kuongoza filamu katika chuo cha New
York Film Academy nchini Marekani, nikimaliza nitaingia kwenye
filamu na kuleta mabadiliko katika uandishi wa hadithi za
filamu hizo tofauti na filamu nyingi za hapa nchini ambazo
nyingi hutambua zinavyoishia baada ya kuitazama mwanzo hivyo
kupoteza ladha ya kuitazama," alisema Millen na kuongeza:
"Movies
zetu za hapa Tanzania zinakosa watunzi wazuri wa hadithi
maana nyingi zikianza unajua zitakapoishia,hivyo tunatakiwa
tujuane na wasanii mbalimbali kutoka nchi mbalimbali kama
ninavyowafahamu baadhi yao kutoka nchini Nigeria na baadhi ya
wasanii wakubwa nchini Marekani ndipo filamu zetu zitafika
mbali," anasema Millen.
Pia
mrembo huyo alifafanua sababu inayomfanya asishuke katika
tasnia ya urembo akidai inatokana na kujituma kwake, kujifunza
zaidi na kutoridhika na mafanikio aliyoyapata huku akiongeza
kwamba anaishi na kuwaheshimu vizuri wanaomuongoza pamoja na
watu wote wanaomzunguka hasa nchi yake.
