KENYA YASHAMBULIWA TENA, WATU WATANO WAPOTEZA MAISHA USIKU WA KUAMKIA LEO

WATU watano wamepoteza maisha baada ya shambulio lililotokea usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Pandanguo huko Witu wilayani Lamu nchini Kenya kilometa 30 kutoka Mpeketoni yalipotokea mauaji ya watu zaidi ya 60 wiki iliyopita.

Polisi wamesema kuwa waliouawa ni kutoka jamii mbalimbali.

Mkuu wa Polisi nchini Kenya, David Kimaiyo amesema kuwa washambuliaji walivamia kijiji cha Pandanguo na kuua takribani watu watano.

"Bado tunawasaka waliohusika na shambulio hili, habari zaidi zitatolewa baadaye," alisema Kimaiyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo