HOTUBA YA RAIS WA ZANZIBAR DKT SHEIN KUMUENZI DAVID LIVINGSTONE MIAKA 141 TANGU KUKOMESHWA BIASHARA YA UTUMWA



Ndugu Wananchi,

Tuna wajibu mkubwa wa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa afya na uzima tukaweza kujumuika leo hii. Napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa viongozi wa Kanisa la Anglikana wa Dayosisi ya Zanzibar na waumini wote wa Kanisa hili kwa kunialika kuja kuungana nanyi katika uzinduzi wa kongamano la kumuenzi Dk. David Livingstone kwa kutambua mchango wake katika kukomesha biashara ya utumwa.
 

Napenda kutoa pongezi kwa maandalizi mazuri ya kongamano hili pamoja na uteuzi mzuri wa mada ambazo zimeandaliwa kuwasilishwa na baadae kuchangiwa na washiriki wa kongamano hili.
 
Nawapongeza wahadhiri wote waliochaguliwa kuwasilisha mada katika kongamano hili kwa heshima kubwa waliyopewa. Kadhalika, napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha wageni wetu wote waliotoka nje ya Zanzibar kuja kushiriki kwenye Kongamano hili. Wote nawashauri watumie fursa hii kutembelea na kuona maeneo mbali mbali ya kihistoria na utajiri wa maumbile ambao Mwenyezi Mungu ameitunukia Zanzibar.
 

Ndugu Viongozi na Ndugu Wananchi,
Sote tuna wajibu wa kuwapongeza marafiki wa Dk. David Livingstone (FDDL) kwa kubuni utaratibu huu wa kufanya maadhimisho ya miaka 141 tangu kukomeshwa kwa biashara ya utumwa hapa Zanzibar. 
Vitabu vya historia vinaeleza kuwa Soko Kuu la Watumwa la Afrika ya Mashariki lililokuwepo hapa Zanzibar, lilifungwa rasmi tarehe 06 Juni (tarehe ya leo) mwaka 1873. Hatua hiyo ina mchango muhimu unaotokana na wamishionari wa madhehebu ya UMCA pamoja na juhudi za Dk. David Livingstone.
 

Nimefurahi kusikia kuwa utaratibu huu wa kufanya maadhimisho haya kila mwaka ni wa kupokezana ambapo mwaka jana; 2013 ilikuwa ni zamu ya wenzetu wa Bagamoyo na mwaka huu wa 2014 ni zamu ya Zanzibar. 
 
Hali hii inadhihirisha kuwepo kwa uhusiano mkubwa wa kihistoria baina ya wananchi wa Tanzania Bara yakiwemo maeneo ya mwambao kama vile Bagamoyo. 
 
Vile vile, hali hii ni kutokana na nafasi ya Zanzibar kuwa ni kitovu cha ziara za wageni wengi kupitia hapa katika ziara zao za maeneo mbali mbali ya Afrika Mashariki na Kati kama ilivyokuwa kwa Mmishionari huyo, Dk. David Livingstone aliyepita Zanzibar kati ya mwaka 1853 na 1856.

<<BONYEZA  HAPA  KUENDELEA  KUISOMA>>

Hotuba  ni  Ndefu, Ingia  hapo  juu  kuendelea  nayo .


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo