Msanii 'kiwango' wa filamu nchini Kulwa Kikumba 'Dude' amekanusha taarifa za kuwepo kwa imani za kishirikina katika misiba inayoikumba tasnia ya Filamu kwa kipindi cha mwezi mmoja sasa.
Dude
amesema kuwa, katika vifo hivyo vya wasanii hakuna uchawi
wowote unaohusika kama watu wengi wanavyosema ambapo amedai
kuwa vifo hivyo vimekuwa vikishtusha sana watu kutokana na
umaarufu wao....
"Sisi
ni kioo cha jamii ndio maana watu wengi wamekuwa na imani za
ajabu kama hizo, ukweli ni kwamba hakuna Uchawi wowote, ni
mapenzi ya Mungu tu.Kikubwa ni kumwamini Mungu kwa kuwa yeye
ni muweza wa yote, alisema Dude
