DEREVA WA BAJAJ AGONGA MTEMBEA KWA MIGUU AKIMBIA KISHA ATIWA MBARONI NA WANANCHI

Msichana ambaye amegongwa na Bajaj hiyo akilia na kujishika katika sehemu za mwili wake.
Mashuhuda wa ajari hiyo wakijaribu kumsaidia dada huyo.
 
Dereva mmoja wa pikipiki aina ya Bajaj ambaye jina lake halikuweza kujulikana mara moja, amemgonga msichana mmoja ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake ambaye alikuwa akivuka barabara.
Ajali hiyo imetokea leo mchana maeneo ya karibu na Chuo cha Ustawi wa Jamii, Mwenge Bamaga jijini Dar, ambapo binti huyo alikuwa akivuka Barabara ya Shekilango  na kugongwa na Bajaj hiyo.
Dereva huyo wa Bajaj baada ya kugonga alitimua mbio na kunza kufukuzwa na wasamaria wema pamoja na dereva daladala na kisha akakamatwa na kuletwa eneo la tukio .
Askari wa Usalama Barabarani alifika eneo hilo na kuanza kuchukua maelezo kwa mashuhuda wa ajali hiyo pamoja na dereva wa daladala linalofanya kazi ya usafirishaji abiria kati ya Mwenge na Kariakoo.
(Picha na Stori Deogratius Mongela /GPL)


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo