MSANII
wa filamu na muziki Bongo, Baby Joseph Madaha (pichani juu) ambaye kwa sasa yuko
Kenya amesema kuwa, haamini kama kweli wasanii wa filamu Recho Haule na
Adam Kuambiana wamefariki dunia mpaka siku atakapoyaona makaburi yao.
Maziko ya Msanii Recho yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar.
Akizungumza na Ijumaa kwa njia ya simu, Madaha alisema ameshitushwa
na vifo hivyo na vimemfanya akose amani kutokana na namna walivyoondoka
duniani ghafla.
Jeneza lenye mwili wa marehemu Adam Kuambiana.
“Nilitamani sana kuwepo lakini niko mpakani mwa Kenya na Uganda kuna
ziara maalum ya kikazi naifanya.
Yaani bado siamini kama kweli
wamefariki, mpaka nije nione walipozikwa,” alisema Baby Madaha.
>>>>GPL


