BAADA YA MASHAMBULIZI KADHAA KUIANDAMA KENYA, SERIKALI YAWATAKA WANANCHI KUANGALIA KOMBE LA DUNIA NYUMBANI KWAO



Serikali ya Kenya imewataka wananchi kuangalia mechi za michuano ya kombe la dunia katika maeneo ya majumbani badala ya sehemu za wazi zilizojazana na ambazo hakuna ulinzi.
 
Ushauri huo umetolewa kufuatia siku mbili za mashambulizi katika mji wa Pwani wa nchi hiyo na kusababisha vifo vya watu 60.
Mashambulizi hayo yalianzia katika eneo la Mpeketoni ambako mashabiki walikuwa wakiangalia mpira siku ya Jumapili.
 
Waziri wa usalama wa ndani amesema licha ya kuwa ulinzi umeimarishwa katika maeneo mbalimbali nchini, wamiliki wa baa na migahawa wanatakiwa kuchukua tahadhari zaidi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo