Kama
hujawahi kusafiri kwenda mikoa ya kusini naomba nikusafirishe kwa picha
hizi ambazo zinaonyesha hali ya kipande kibovu kinachowakalisha muda
mwingine kwa zaidi ya masaa 10 wasafiri wa mikoa ya kusini hasa
inaponyesha mvua ambapo hali ya sehemu hii hua inapitika kwa shida sana.
Kuna kipindi bidhaa hupanda hasa kwa sehemu kama
Lindi,Mtwara,Masasi,Nachingwea,Newala,Tandahimba na baadhi ya sehemu
ambazo hutegemea barabara hii kusafirishia bidhaa na abiria,hizi ni
picha kadhaa zinazoonyesha eneo hili inapotokea barabara inapokua
imeharibika.
CHANZO:MILLARDAYO.COM
