WAKULIMA WAMLALAMIKIA KINANA JINSI WANAVYOLAZIMISHWA KUUZA TUMBAKU KWA VYAMA VYA USHIRIKA


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Ufuluma wilaya ya Uyui  ambapo aliwaambia wananchi hao Kilimo cha Tumbaku kiondoe umasikini na si kuongeza umasikini kwa mkulima.

Wakulima wa Tumbaku kata ya Ufuluma wamelalamikia kulazimishwa na viongozi wa vyama vya ushirika kuuza tumbaku yao katika vyama hivyo ,hata kama sio wanachama.Kinana amewataka wakulima hao kutokukubali kusumbuliwa kuuza tumbaku yao katika vyama hivyo ambavyo baadhi yake vimejaa walaghai na wanyonyaji wa wakulima hao.

Amesema kuwa Wakulima wa zao hilo la tumbaku wamekuwa wakifanya kazi kubwa na ngumu,lakini hawafaidika na jasho la kazi yao,kutokana na kuanzishwa kwa vyama vingi vya ushirika ambavyo vipo kwa faida ya wajanja wachache,hivyo wakulima hao wasilazimishwe kuuza tumbaku yao kwa vyama vya ushirika.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh Fatma Mwasa aliongeza kuwa mnamo mwaka 2012 wakulima wa Tumbaku waliibiwa kiasi cha fedha shilingi Bilioni 16,kama vile haitoshi mnamo mwaka 2013 wakulima hao waliibiwa kiasi cha fedha shilingi bilioni 12 na umoja wa vyama vya ushirika,akabainisha kuwa kufuatia ubadhilifu huo mkubwa wa fedha kwa wakulima,mwaka huu tumbaku haitatolewa kienyeji kwa vyama hivyo mpaka wahakikishiwe fedha zao zitalipwaje.


Akabainisha kuwa imefika wakati wakulima wa Tumbaku wajitegee,wawe huru na kuamua ni wapi wauze tumbaku yao na kwa bei waitakayo ni si kupangiwa na vyama vya ushirika,akaongeza kwa kusema kuwa Wakulima hao wasilazimishwe kuuza tumbaku yao kwa Vyama vya ushirika. 

Kinana amemaliza ziara yake wilayani Uyui leo  na kesho ataunguruma wilayani Sikonge mkoani Tabora. 
 Wakazi wa Ufuluma wakishangilia na wengine wakifuatilia jambo kwenye mkutano uliofanyika leo kwenye kata hiyo ya Ufuluma,wilayani Uyui mkoani Tabora.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo