Waziri
wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (kushoto) na Chris Sattler,
Afisa Mtendaji Mkuu wa Uranium One, (wa pili kushoto) wakisaini Mkataba
wa Makubaliano (MoU) ambao inairuhusu kampuni ya uchimbaji madini ya
urani ya Mantra Tanzania kuwekeza dola za Kimarekani 800,000 katika
mwaka 2014 itakayo tumika katika shughuli za kupambana na ujangili
katika mbuga za wanyanya nchini Tanzania. Aliyesimama ni Galina
Molchanova, Makamu wa Rais wa kamapuni ya Mantra Tanzania. Hafla hiyo
fupi ilifanyika sambamba na mkutano wa siku mbili wa Wanyamapori
uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
========= ========
Dar es
Salaam, Tanzania – KAMPUNI ya Mantra Tanzania na Idara ya Wanyamapori
ya Wizara ya Maliasili na Utalii (Wildlife Division) wamesaini mkataba
wa makubaliano, ambao umelenga kwa pande zote mbili kushirikiana katika
kupiga vita ujangili wa tembo katika eneo la kusini mwa hifadhi ya
wanyamapori ya Selous. Katika makubaliano hayo, kampuni ya
Mantra Tanzania itawekeza Dola za Kimarekani laki nane ($ 800,000)
katika mwaka 2014 katika kampeni dhidi ya ujangili nchini.
Makubaliano
hayo yalisainiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Uranium One Inc Bw. Chris Sattler kwa
niaba ya Mantra Tanzania (kampuni dada ya Uranium One ambayo inasimamia
mradi wa Mto Mkuju, mgodi mkubwa duniani wa uranium katika ukanda wa
kusini wa nchi). Hafla ya kusaini makubaliano hayo ilifanyika sambamba
na mkutano wa siku mbili wa Wanyamapori uliofanyika jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki.
“Ujangili
wa ndovu umefikia hatua mbaya katika hifadhi ya wanyamapori ya Selous
na kampuni ya Mantra imejipanga kikamilifu kuchukua hatua madhubuti ili
kukabiliana na tatizo hili,” alisema Bw. Sattler. Aliongeza,
“Makubaliano haya yanaturuhusu kushirikiana na Idara ya Wanyamapori,
kuandaa na kuutekeleza mpango wa kupiga vita ujangili ili kuwaokoa ndovu
waliopo katika hifadhi ya Selous. Napenda kumshukuru Waziri Nyalandu
kwa uongozi wake katika suala hili la msingi. Najua wote tunamatumaini
kuwa mpango huu utasaidia kuonyesha njia kwa makampuni binafsi na ya
umma kushirikiana katika kuhifadhi wanyamapori Tanzania na Afrika.”
Kwa
upande wake, Waziri Nyalandu alisema serikali ya Tanzania, ambayo
inaunga mkono Mradi wa Mto Mkuju, itajitahidi kuhakikisha kwamba masuala
mengine yaliyosalia kusainiwa yatasainiwa ikiwa ni pamoja na
Makubaliano ya Uchimbaji Madini na uendelezaji wa migodi (Mining
Development Agreement -MDA-) inatekelezwa kabla ya mwisho wa mwaka wa
fedha unaoishia mwezi Juni.
“Jitihada
zinazoambatana na hati hii ya kulinda na kutusaidia kupambana na
ujangili katika hifadhi ya wanyamapori ya Selous na pia kupiga hatua
zaidi na kuanzisha Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania zitakuwa na maana
mara baada ya kusaini MDA. Nategemea kushirikiana na wenzangu toka
Wizara ya Nishati na Madini na Wizara ya Fedha kuhakikisha kuwa
tunayafanyia kazi utaratibu zilizobakia ili mradi huo
uanze uzalishaji. “Kwa kusaini makubaliano haya,
ninaonyesha njia ya kuwa ni suala linalowezekana kwa seka binafsi na ya
umma kufanyakazi kwa pamoja ili kufikia lengo linalokusudiwa,” alisema
Nyalandu.
Kwa
mujibu wa makubaliano hayo, kamati maalum itakayojumuisha wawakilishi
wawili kutoka Mantra na wengine wawili kutoka katika Idara ya
Wanyamapori itaundwa. Kamati hiyo itakuwa na jukumu la kuandaa,
kutekeleza na kuufanyia tathmini mpango huo wa kupiga vita ujangili, na
pia kwa ajili ya kuwasiliana na wadau mbali mbali, ikiwa ni pamoja na
wawakilishi toka katika ngazi zote za serikali, jamii, makundi ya
wawindaji na mashirika yasiyo yakiserikali.
Mkataba
huo umejikita zaidi katika kuuendeleza mpango wa vita dhidi ya
ujangili, ambao kampuni ya Mantra Tanzania ulishauanza mwaka 2013. Chini
ya mpango huu, wahitimu 20 kutoka Chuo cha Mafunzo ya Uaskari
wanyamapori cha hifadhi ya Selous wataingizwa katika kitengo cha kampuni
ya Mantra cha kupiga vita ujangili. Makubaliano hayo
yanaeleza kuwa askari watabaki kuwa wafanyakazi wa hifadhi ya Selous na
kurudishwa katika hifadhi baada ya miezi 12 ya kufanya kazi. Wakati
kitengo cha kupiga vita ujangili cha Mantra, askari watapatiwa hifadhi
karibu na Mradi wa Mto Mkuju na kufanya patroo katika eneo lenye
kilometa za mraba 20,000 kuzunguka eneo la mradi.
Mantra
itawapatia askari hao mavazi, vifaa na vyombo vya usafiri, pamoja na
mafunzo maalum katika mawasiliano, usalama, utafutaji uelekeo na mbinu
za kukabiliani na ujangili. Kufanya uchunguzi kwa kutumia ndege maalum
inaandaliwa na majaribio ya kutumia magari maalum yenye kamera
zitumikazo usiku GPS navigation na video transmitters vimeshakamilishwa.
Kufuatana na kufuata taratibu na ruhusa zinazotakiwa, shughuli hizi za
ulinzi, zinazounga mkono vita dhidi ya ujangili vitaundwa na kuanza
kazi.
Shughuli
za Mantra za kupiga vita ujangili pia zitaenda pamoja na mitandao ya
ukusanyaji taarifa ya jamii, ambayo itasaidia katika kukusanya,
kuchambua na kutoa taarifa juu ya shughuli za ujangili.
