MCHUMBA ambaye alifikia hadhi ya mume wa mwigizaji
marehemu Sheila Haule ‘Recho’, George Sagunda amefunguka kuwa
amechukizwa na watu wasiojulikana kuweka picha feki ya marehemu
mitandaoni.
Akizungumza na mtandao huu, Saguda alisema muda mchache baada ya
mazishi yaliyofanyika wiki hii, watu wasiojulikana waliweka picha ya
marehemu akiwa na mwanaye kwenye jeneza kitu ambacho siyo sahihi.
“Imeniuma sana,
wamefojifoji picha na kuweka kichanga ambacho siyo chenyewe kisha
kuposti katika mitandao wakidai ni marehemu Recho na kichanga chake,
wasifanye hivyo jamani…,” alisema Saguda.