Umati wa watu ukiwa unashangaa kitendo cha mwanadada (kushoto mwenye kitambaa cha zambarau kichwani) aliyemkwapulia 20,000 mwenzake.
MWANADADA mmoja ambaye jina lake halikufahamika amejikuta akinusurika
kupigwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kumuibia mama aliyekuwa
na mtoto.
Ishu nzima imetokea maeneo ya jirani na hospitali ya Amana, Ilala,
jijini Dar es Salaam, ambapo baada ya mama mmoja aliyekuwa na mtoto
kumkabidhi mwanadada (mwizi) mtoto na mkoba wake, ndipo mdada huyo
alipochomoa shilingi 20,000/= kwenye mkoba wa mama huyo.
Aliporudi mama wa mtoto alimkabidhi mtoto na mkoba wake kisha
kuondoka kwa haraka na wasiwasi mwingi, kitu kilichomshitua yule mama na
kujisachi ndipo alipobaini kuibiwa na kuanza kupiga kelele za mwizi.
Vijana walionyesha uwezo wao kwa kumkimbiza na kumkamata ambapo
alinyang’anywa pesa na zogo likaibuka wakati wengine wakitaka kumpiga
huku baadhi ya vijana wakionekana kumkingia kifua kwa kuwa ni mwanamke.
(Picha na Gabriel Ng’osha/GPL)