MTANGAZAJI MAHIRI REUBEN MCHOME AACHA KAZI ITV/RADIO ONE STEREO

Taarifa ambazo zimetufikia leo hii ni kwamba mtangazaji maarufu wa radio one na ITV Reuben Mchome ameacha kazi rasmi katika vituo hivyo maarufu vya habari hapa nchini.
 
Jembe hilo limeacha kazi rasmi Ijumaa ya tarehe 09-05-2014 kwa madai kwamba anakwenda kujiendeleza na masomo.
 
Jitihada za kumpata Reuben Mchome mwenyewe ili kuthibitisha hili zilizaa matunda Japo hakuwa tayari sana kulizungumzia suala hilo,ila baada ya kubanwa na maswali alifunguka na kuzungumza.
 
Yafutayo ni mazungumzo yetu na mtangazaji huyo kijana ila mwenye kipaji cha hali ya juu,Reuben Mchome.
 
Eddy Blog-Mambo vipi Mchome.
 
Mchome-poa mambo vipi?
 
Eddy Blog-poa asee!! Nasikia umeacha kazi ITV,Ni kweli?
 
Mchome- Wee nani?
 
Eddy Blog-mwandishi wa habari wa Eddy blog!!
 
Mchome- wee nani kakwambia kama mimi nimeacha kazi?
 
Eddy Blog-Nimesikia watu wakiongea,Si uanajua nyie ni watu maarufu lazima mambo yenu yasambae kwa haraka!!
 
Mchome-sasa kama umesikia kwa watu unachotaka kwangu ni nini?
 
Eddy Blog-tunaomba ututhibitishie kama ni kweli au la!!?
 
Mchome- ni kweli nimeacha kazi
 
Eddy Blog-umefukuzwa au umeamua mwenyewe?
 
Mchome-(anaanza kwa kicheko) hapana sijafukuzwa nimeamua mwenyewe kuacha!! 
 
Eddy Blog-umepata dili wapi?
 
Mchome-sijapata popote nimeamua kuacha ili nimalizie shule yangu.
Eddy Blog- ooooh!! Kumbe unasoma,unasoma wapi? 
 
Mchome-Nipo chuo kikuu Tumaini
 
Eddy Blog-mwaka wa ngapi?
 
Mchome-wa tatu!!
 
Eddy Blog-kwahiyo ukimaliza utarudi kazini au ndio umetoka moja kwa moja?
 
Mchome-(anaanza kwa kicheko tena) hapana kaka siwezi kurudi tena!!
 
Eddy Blog-lakini inasemekana ulitofautiana kauli na "boss" wako ndio maana ukaamua kucha kazi ndani ya saa ishurini na nne!!
 
Mchome-(anastuka) Eh!! Wewe nani kakuambia hayo?
 
Eddy Blog-aaa kaka si unajua mwenyewe dunia siku hizi imekuwa kama kijiji!?
 
Mchome- katika hilo kaka nakuomba sana usije ukanipandikizia maneno!! Mimi sijatofautia na boss wangu yoyote pale, mimi nimeondoka kwa amani na maboss wangu wote nimeagana nao kwa amani na upendo nakuomba sana kaka unielewe hivyo!
 
Eddy Blog- sawa kaka, ila kuna taarifa kwamba mkurugenzi wako Deogratius Rweyunga alikukatalia likizo yako ya kwenda kufanya mitihani yako ndiyo maana ukaamua kuacha kazi!!
 
Mchome-hayo ni majungu kaka,wewe umesema umesikia kwamba nimeacha kazi ndio maana ukaamua kunipigia kuthibitisha hilo,naomba uandike ninachokuambia mimi!! Sijanyimwa likizo wala sijatofautiana na aliyekua boss wangu,huyo aliyekuambia ni mzushi na muongo!
 
Eddy Blog-lakini kaka inasemekana umepata dili kwenye kituo kimoja cha TV na Radio hapa nchini,ni kweli?
 
Mchome-sio kweli,sijapata dili na kwa sasa sitaki dili lolote hadi nitakapo maliza degree yangu mwezi wa saba.
 
Eddy Blog-lakini ukimaliza shule unatarajia kuendelea na kazi hii ya habari au ndio umeitema kabisa?
 
Mchome-dah sujajua kaka,unajua maisha ni hatua,ngoja nimalize shule kaka kitaeleweka tu.
 
Eddy Blog-basi naomba nikupe dili ukimaliza shule uje nikupatie ajira hapa Eddy Blog
 
Mchome-(anacheka kicheko kirefu) Poa poa kaka kama utakua na mkwanja wa kunilipa nitakuja usijali.
 
Eddy Blog-poa kaka nashukuru kwa kuzungumza na Eddy Blog na tunakutakia kila la kheri katika masomo yako na maisha mapya nje ya Radio one na ITV
 
Mchome-poa poa kaka tupo pamoja.
 
Hayo yalikuwa mazungumzo kati yetu na Reuben Mchome,katika vituo hivyo maarufu vya habari vya ITV na Radio One 
Reuben akiwajibika kwenye studio za redio One enzi hizo.
 
Reuben Mchome kwa upande wa Radio alikua anasoma taarifa za habari, kipindi cha Nipashe, Midundo motomoto, Afrika Panorama, Breaking News na Uchunguzi kamili, kwa upande wa TV alikuwa anasoma habari za michezo.
 
Eddy Blog inamtakia Reuben Mchome kila la kheri katika masomo yake na inawapa pole mashabiki na wapenzi wake ama kweli wataikosa sauti iliyozoeleka masikioni mwao!!


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo