Kwa mlio uliotokea na jinsi tukio lenyewe lilivyokuwa Walter alipata
mshtuko na kupanic kwa muda kabla ya kuanza kurejea kwenye hali yake
kutokana na ajali hii ambayo haikumpa jeraha lolote.
Kwa jinsi jamaa wa gari jingine alivyomvamia unaweza kuhisi labda
alikua anayo nia ya kumuumiza Walter au alipania kumgonga isivyo kawaida
manake toka alipokuwa nyuma ya Walter alikua akimuwashia taa kwa mwanga
mkubwa kuashiria anataka kupita.
Walter anasema ‘wale jamaa ilikua kama wanakimbizwa huko walikotoka’Uwapo barabarani Dar es salaam unashauriwa kumpisha yeyote anaetaka
kupita kama kuna nafasi, Mwaka jana kuna dereva wa daladala aliuwawa kwa
risasi na watu waliokua kwenye pikipiki waliotaka awapishe lakini akawa
anawanyima nafasi ambapo walipopata upenyo wa kumpita eneo la Sinza
Kumekucha jamaa aliekua kapakiswa kwenye pikipiki alifyatua risasi
iliyomuua palepale dereva wa daladala.
Kabla ya kumuua yalitokea majibizano kidogo ambapo iliripotiwa Dereva
wa daladala kama kawaida yao akajibizana nao na kuwauliza watamfanya
nini, wasepe zao waache kumbabaisha.
CHANZO:millardayo.com
