MAUMIVU! Mfugaji wa jamii ya Kimasai, Sita Lumembe (36), mkazi wa Kijiji cha Ludewa wilayani Kilosa mkoani hapa, amefikishwa hospitalini akiwa hoi baada ya kupigwa pembe la tumbo na mmoja wa ng’ombe wake aliokuwa akiwachunga.
“Ng’ombe wake mmoja aliyekuwa na ndama alimpiga na pembe tumboni, akaanguka na kupoteza fahamu.
“Wasamaria wema walinipigia simu, nikafika eneo la tukio na kukodi bodaboda iliyomkimbiza hospitalini.
“Baada ya daktari kumcheki, alikimbizwa wodini kwani damu ilikuwa
ikimwagika kwa wingi kutoka tumboni,” alisema Lumembe akiwa na huzuni.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kilosa, Christopher Chiweka alithibitisha kumpokea mgonjwa huyo.
“Alifikishwa akiwa na hali mbaya mno hivyo tukamkimbiza wodini kwa uchunguzi zaidi, sambamba na matibabu anayoendelea nayo,” alisema daktari huyo.
“Alifikishwa akiwa na hali mbaya mno hivyo tukamkimbiza wodini kwa uchunguzi zaidi, sambamba na matibabu anayoendelea nayo,” alisema daktari huyo.