TAARIFA KWA UMMA
Mfuko wa Pensheni wa PSPF unapenda
kuwataarifu wananchi wote kuwa, hivi karibuni kumekuwa na watu au
kikundi cha watu wanaosambaza taarifa potofu kwa wanachama wa PSPF kwa
njia ya ujumbe mfupi wa simu ya mkononi kwa nia ya kuwatapeli.
Taarifa hizo zinazotolewa siyo sahihi na PSPF inawaomba wanachama
wake kuchukua tahadhari dhidi ya ujumbe huo wa kupotosha unaosambazwa
kwa njia ya simu na watu au kikundi cha watu wakidai kuwa ujumbe huo
unatoka PSPF.
PSPF inatoa huduma mbalimbali kwa wanachama wake bila sharti lolote
wala malipo ya namna yoyote. Ujumbe wowote unaomtaka mwanachama kutuma
fedha kwa ajili ya kulipia huduma yoyote inayotolewa na Mfuko siyo
sahihi na ujumbe wa namna hiyo hautolewi na PSPF. Hivyo, ninawaomba
wanachama wa PSPF kuwa makini na ujumbe huo unaosambazwa na watu
wachache ambao wanataka kuuchafua Mfuko na kujinufaisha kwa njia zisizo
halali.
Iwapo itatokea mwanachama amepata ujumbe wenye utata, tafadhali piga
simu katika Kituo cha Huduma kwa Wateja wa PSPF kwa kutumia namba 022
5510400 au fika katika ofisi ya PSPF iliyopo karibu nawe au toa taarifa
kituo chochote cha polisi kilicho karibu nawe kwa hatua stahiki.
Taarifa hii imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Mfuko wa Pensheni wa PSPF,
Makao Makuu, Golden Jubilee Towers, S. L. P. 4843, Dar-es-Salaam.
Simu: +255222120912/52 au +255222127375 /6
Nukushi: +255222120930
Barua pepe: pspf@pspf-tz.org
Tovuti: www.pspf-tz.org
www.facebook.com/PSPFTanzania
@Pspf_Tanzania
Taarifa hii imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Mfuko wa Pensheni wa PSPF,
Makao Makuu, Golden Jubilee Towers, S. L. P. 4843, Dar-es-Salaam.
Simu: +255222120912/52 au +255222127375 /6
Nukushi: +255222120930
Barua pepe: pspf@pspf-tz.org
Tovuti: www.pspf-tz.org
www.facebook.com/PSPFTanzania
@Pspf_Tanzania
