MBARONI KWA KOSA LA KUPOKEA NA KUSAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU MKOANI MBEYA



POLISI Mkoani Mbeya, inamshikilia mtanzania mmoja Hamis Mwakalinga(29) mkazi wa eneo la Soweto Jijijini Mbeya, kwa tuhuma za kuwapokea na kuwasafirisha wahamiaji haramu 17.

Akizungumza jijini Mbeya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa saba mchana eneo la Mwanjelwa stendi ya Tukuyu Kata ya Ruanda Jijini Mbeya.

Amesema, polisi walipata taarifa ya kwamba mtanzania huyo yupo na wageni kutoka nje kwenye eneo hilo akihangaika kuwasfirisha.

Amesema mara baada ya kupata taarifa hizo Polisi waliweka mitego na baadaye kumbaini mtuhumiwa huyo akiwa na wahamiaji haramu hao.

Kamanda Msangi, amemtaja mmoja wa  raia hao kuwa ni Nyabeda Samsoni (32) ambaye alikuwa na wenzake 16.

Aidha, amesema kuwa wahamiaji haramu hao tayari wamekabidhiwa kwenye mamlaka husiaka ya uhamiaji.

Hata hivyo, Kamanda Msangi ameiomba jamii kuondokana na tamaa zisizokuwa na ulazima kwani kitendo cha kuwapokea raia wakigeni kwa kificho kinaweza kikaligharimu Taifa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo