Madiwani
wa Chama cha CUF,wilayani Urambo wakimpokea kwa bashasha kubwa katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwasili katika wilaya ya
Urambo,mapema leo akitokea wilayani Sikonge.Shoto ni Diwani wa
CUF,Mh.Kandola Nyanda wa kata ya Nsenda na kati ni Diwani wa CUF,Kata ya
Usoke,Mh.Kadada Mohamed,ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya
elimu,afya na maji katika halmashauri ya Urambo mkoani Tabora.Pichani
nyuma ya Kinana ni Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Ndugu Nape
Nnauye akifurahia jambo.
Diwani
wa CUF,Mh.Kandola Nyanda wa kata ya Nsenda akimpokea kwa bashasha kubwa
katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwasili katika wilaya ya
Urambo,mapema leo akitokea wilayani Sikonge.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora,Mh Fatma Mwasa akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la
Urambo,Mh.Samwel Sitta mara baada ya kuwasili kwa Katibu Mkuu wa
CCM,Ndugu Kinana Wilayani Urambo mapema leo.
Mbunge wa Urambo Mashariki Mh.Samwel Sitta akimkaribisha katika jimbo lake Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake mapema leo.
Katibu Mkuu wa CCM ,Ndugu Kinana akizungumza jambo na Mbunge wa Urambo Mashariki Mh.Samwel Sitta,Pichani kati ni Mkuu wa Mkoa,Mh.Fatma Mwasa pamoja na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye.
Katibu Mkuu wa CCM ,Ndugu Kinana pamoja na Mbunge wa Urambo Mashariki Mh.Samwel
Sitta wakishiriki ujenzi wa jengo la maabara katika shule ya sekondari
Uyumbu,katika kata ya Uyumbu wilayani Urambo mkoani Tabora-
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Ujumbe wake wakielekea kwenye ukaguzi wa
mradi wa jengo la Zahanati ya Izengatogilwe,Wilayani Urambo.Zahanati
hiyo itakuwa ina uwezo wa kuhudumia watu wapatao zaidi ya Elfu
mbili,kutoka kijiji cha Izenga,Tebela,Msumbiji na Isongwa.
Ndugu Kinana akitoka kukagua moja ya chumba cha zahanati hiyo ya Izengatogilwe,Wilayani
Urambo,yenye uwezo wa kuhudumia watu wapatao zaidi ya Elfu
mbili,kutoka kijiji cha Izenga,Tebela,Msumbiji na Isongwa.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pichani kati,shoto ni Mbunge wa Urambo Mashariki Mh.Samwel Sitta pamoja na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye wakipata picha ya pamoja na kikundi cha Sungu Sungu
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiweka jiwe la msingi kwenye mradi wa akina
mama,mashine kati ya nne za kukamulia mafuta ya Alizeti,Wilayni Urambo
mkoani Tabora
Ndugu Kinana akipata maaelezo mafupi ya mradi huo wa mashine ya kukamulia Alizeti
Ndugu
Kinana akikagua shamba la mahindi linalomwagiliwa kwa njia ya
Matone,linalomilikiwa na kikundi cha Hiyari ya Moyo kilichopo katika
kijiji cha Ndolobo,Wilayani Urambo.
Ndugu Kinana akikagua mradi wa ujenzi wa jengo la wodi ya akina Mama Wanaosubiri kujifungua,liitwalo Mayulindila.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na vijana wa chipukizi
wa CCM,katika mpaka wa Sikonge na Urambo,katika kijiji cha
Izimbili,tarafa ya Usoke Wilayani Urambo kwa ziara ya siku mbili,ambayo
itaambatana na wilaya ya Kaliua mkoani Tabora,ambapo Kinana atakuwa na
ziara ya siku 11 mkoni humo,ambapo kilele chake itakuwa siku ya
jumapili,ambapo mkutano wa hadhara utafanyika.
















