KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA DARAJA LA MBUTU WILAYANI IGUNGA LEO.



 Meneja Mradi wa ujenzi wa Daraja la Mbutu,Injinia Makoye Luhuya akielezea maendeleo ya ujenzi wa daraja la Mbutu kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mapema leo,wilayani Igunga mkoani Tabora
 Ujenzi wa daraja la Mbutu ukiendelea kwa kasi
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiweka mbao wakati wa ujenzi wa daraja hilo ukiendelea,wilayani Igunga mkoani Tabora mapema leo asubui.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa  Meneja Mradi wa ujenzi wa Daraja hilo,Injinia Makoye Luhuya kuhusu ujenzi wa daraja la Mbutu, wilayani Igunga, leo Mei 9, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kuimarisha uhai wa chama na kusikiliza kero za wananchi mkoani Tabora. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (mbele) akishuka, baada ya kukagua ujenzi wa daraja la Mbutu, wilayani Igunga, leo Mei 9, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kuimarisha uhai wa chama na kusikiliza kero za wananchi mkoani Tabora. 
 Sehemu ya Daraja hilo Mbutu kama lionekanavyo pichani.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo