Meneja Biashara ya Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Julius Gashaza enzi za uhai wake.
JAMBO limezua jambo! Maswali matano ya msingi yameibuka kufuatia kifo
cha aliyekuwa Meneja Biashara ya Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa
Nishati na Maji (Ewura), Julius Gashaza kilichotokea hotelini katika
mazingira ya kutatanisha muda mfupi baada ya kuwasili jijini Dar akitoka
Dodoma ambako alihojiwa na Kamati ya Bunge ya Bajeti, Amani limeyanasa.
Habari za kiintelijensia zilidai kwamba marehemu Gashaza ndiye
aliyekuwa na majukumu ya kupanga bei za mafuta kila mwezi, alikuwa mjini
Dodoma kwa siku mbili, Ijumaa na Jumamosi iliyopita kuhusu kuweka wazi
kiwango cha mafuta kinachoingizwa nchini, mgawo wa fedha unaotolewa na
Ewura kwenda kuhudumia umeme katika vijiji (Rea) na fedha za mfuko wa
barabara.
Jumapili iliyopita, meneja huyo alikutwa amekufa kwenye Hoteli ya
Mwanga Lodge iliyopo Yombo-Vituka, wilayani Temeke jijini Dar na
kusadikiwa kuwa alijinyonga kwa tai kwenye nondo za dirisha la chooni
katika chumba Na. 113.Mwandishi wetu alifuatilia kwa karibu tukio hilo
la kusikitisha na kubaini mambo kadha wa kadha.
Jumatatu iliyopita mwandishi wetu alianza kwa kufika nyumbani kwa marahemu lakini hakuna aliyekuwa tayari kutoa ushirikiano mwa mwanahabari wetu.
Baada ya hapo, mwandishi wetu alikwenda kwenye hoteli hiyo ambako ndiko alikopata maswali hayo matano yenye kuumiza kichwa.
Mhudumu mmoja wa hoteli hiyo ambaye aliomba hifadhi ya jina, alisimulia mazingira yote ya kifo cha meneja huyo, alisema:
“Usiku wa kuamkia siku ya tukio, marehemu alikuja hapa hotelini akiwa ameongozana na watu wanne. Wanawake wawili na wanaume wawili akiwemo yeye marehemu.
“Nilisikia wale wanawake mmoja alikuwa mke wa marehemu, mwingine mke wa rafiki wa marehemu. Wakachukua chumba, wakaingia ndani wote.
“Baada ya muda, walitoka watatu. Mke wa marehemu, rafiki yake na mke wa rafiki yake.
“Kwa hiyo inamaanisha ndani ya chumba alibaki marehemu, maana si waliingia wanne na wametoka watatu!
“Kwa hiyo inamaanisha ndani ya chumba alibaki marehemu, maana si waliingia wanne na wametoka watatu!
“Tulilala! Asubuhi alikuja yule rafiki wa marehemu akasema anaomba
kusaidiwa kumwona marehemu maana amekwenda kugonga lakini hajaamka na
mlango umefungwa.
“Tulikwenda wote, kufika kweli mlango ulifungwa. Ikabidi tuchukue funguo nyingine kufungua.
“Hakuwemo chumbani na kwenye kitanda palionesha alama ya mtu kukaa tu si kulala kwani palitengeneza duara alipokaa.
“Hakuwemo chumbani na kwenye kitanda palionesha alama ya mtu kukaa tu si kulala kwani palitengeneza duara alipokaa.
“Kwenda chooni ndipo tukamkuta amekufa kwa kujinyonga kwa tai.”
Alisema kwamba ndipo taratibu za kuwaita polisi zilifuata.
Alisema kwamba ndipo taratibu za kuwaita polisi zilifuata.
MANENOMANENO YA WATU
Kufuatia hali hiyo, kumeibuka maneno mengi. Wengine wanadai marehemu alinyongwa na wabaya wake, wapo wanaosema alijinyonga kufuatia uchungu wa kutishiwa maisha na wabaya wake kuhusu kazi.
Kufuatia hali hiyo, kumeibuka maneno mengi. Wengine wanadai marehemu alinyongwa na wabaya wake, wapo wanaosema alijinyonga kufuatia uchungu wa kutishiwa maisha na wabaya wake kuhusu kazi.
Wengine wakaenda mbele zaidi kwa kudai kuwa wanyongaji hao walimfuatilia kwa muda mrefu siku ya tukio.
MASWALI MATANO
Swali la kwanza: Kama kweli marehemu alinyongwa ni kwa nini mlango ulikutwa umefungwa kwa ndani? Je, mnyongaji alitokaje baada ya kutekeleza mauaji hayo?
Swali la kwanza: Kama kweli marehemu alinyongwa ni kwa nini mlango ulikutwa umefungwa kwa ndani? Je, mnyongaji alitokaje baada ya kutekeleza mauaji hayo?
Swali la pili: Kama kweli marehemu alinyongwa, kwa nini kitandani
kulikutwa na alama ya mtu kukaa tu na kusiwepo kwa dalili za mapambano
au purukushani?
Swali na tatu: Kama kweli alijinyonga mwenyewe ni kwa nini iwe
kipindi hiki ambacho inadaiwa alipokea vitisho kutoka kwa wabaya wake
kwamba atauawa?
Swali la nne: Uamuzi wa kuchukua chumba kwenye hoteli hiyo ulitoka kwa nani? Marehemu mwenyewe au? Kama alishauriwa, aliyemshauri ana cha kujibu?
Swali la tano: Kama kulikuwa na matatizo ya kikazi kama ilivyodaiwa,
basi Mkurugenzi Mstaafu wa Ewura, Haruna Masebu atakuwa anayajua hivyo
angeweza kusaidia kuyasema.
Swali lingine ambalo lingeweza kuongeza idadi ni juu ya uwezekano wa
kuingizwa kwa funguo nje wakati ya ndani ilizungushwa lakini imebainika
kwamba baada ya funguo kufungwa na mlango kuwa ‘lokdi’, funguo hiyo huwa
‘luzi’ tena hivyo mwenye funguo nje anaweza kuisukuma na kuingiza
nyingine.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Engelbert Kiondo alikiri kutokea
kwa tukio hilio akisema ameshaingiza ‘vijana’ wake kuchunguza ukweli wa
tukio hilo la kujinyonga au kunyongwa.
Mwili wa marehemu Gashaza uliagwa juzi nyumbani kwake, Yombo-Vituka,
Dar na kusafirishwa Ngara, Kagera kwa mazishi. Mungu ailaze pema peponi
roho ya marehemu. Amina.
CHANZO:GAZETI LA AMANI