Halmashauri ya wilaya ya Makete imekusudia kuongeza zawadi kwa wafanyakazi hodari wa halmashauri hiyo kama njia mojawapo ya kutambua kile anachokifanya akiwa kazini.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Afisa Utumishi wa halmashauri hiyo Bw. Nikodemasi Tindwa wakati akijibu hoja ya wauguzi wa hospitali ya wilaya ya Makete walioshauri watumishi wanapofanya vizuri wapongezwe na si kulaumiwa tu.
Mtumishi wa halmashauri ya wilaya ya makete akipokea zawadi ya mfanyakazi hodari kwenye mei mosi ya mwaka huu.
Amesema suala hilo ni nzuri na ndiyo maana katika siku ya Mei Mosi mwaka huu walijitahidi kutoa zawadi kwa watumishi hodari ambao walipewa fedha taslimu sh. laki tatu na kwa sasa wanatarajia kuongeza hadi kufikia sh. laki tano.
Bw. Tindwa amesema suala la kutambua watumishi hodari na kuwapa zawadi halipingiki huku akisisitiza watumishi wote kufanya kazi zao kwa bidii kwa kuwa kila mtumishi hodari katika sekta mbalimbali za halmashauri watatambuliwa na kupewa zawadi