Jeshi
la Polisi Wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi linawashikilia watu watatu kwa
tuhuma za kumuuwa dereva Bodaboda mmoja aitwaye Frenk Joseph (25)mkazi
wa mtaa wa Nsemlwa Wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi kwa kumchinja shigo na
kisha kumpora pikipiki yake aina ya SANLG yenye namba za usajiri T 704
CDQ.
Kamanda wa jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Kamishina
msaidizi mwandamizi Dhahiri Kidavashari aliwataja watuhumiwa hao kuwa
ni Charles Kidaha(29),Madia Mtema (40) na Buyenza Jendesha (40) wote
wakazi waTarafa ya Mwese Wilayani Mpanda.
(Pichani wanaosadikiwa kuwa majambazi waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo).
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi