WILAYA YA MAKETE KUPOKEA WAALIMU WAPYA 179

Na  Festo James  Njombe

Katika Kuhakikisha Tatizo la walimu wa shule  za Sekondari na Msingi  linaendeleaa kuatatuliwa,  Mkoa wa Njombe  Umepokea  Walimu Zaidi ya Mia Nane  Ambao Wameanza Kuripoti Katika  Vituo Vyao vya Kazi  Tangu Hapo Juzi.

Akiongea na blog hii  Afisa Elimu Mkoa wa Njombe  Bw Said Kinyaga Nyasiro  Amesema Kuwa Kati ya Walimu Hao waliopangwa katika Mkoa wa Njombe ni walimu 831 Ambapo Walimu wa  Masomo ya Sayansi ni  54 huku waalimu wa sanaa ni  445  na walimu wengine  ni wa cheti   wakiwa 332.

Aidha Afisa Elimu Huyo Amebainisha Kuwa  Walimu 179 wanaratajia Kwenda Wilaya Ya Makete,132 Wilaya ya Ludewa, 127 Wilaya ya Wanging'ombe na Wilaya ya Njombe Walimu 393 Watakao Sambazwa Kwenye Halmashauri Zake.
 
Bw Nyasiro   Ameongeza Idadi Hiyo ya Walimu imekuja wakati Mkoa wa Njombe Ikiwa na Upungufu wa Walimu  Zaidi ya Elfu Mbili  Hivyo Kuwataka Walimu Hao wapya Kuwasili Katika Vituo Walivyopangiwa Mapema Kama Sheria Inavyosema.

Ameongeza Kuwa Mapokezi Hayo ya Walimu Yanaenda Sanjari na  Uhakiki  wa  Uhalali  wa Walimu Hao Kwa Kuachunguza Vyeti Vyao.
 
Katika Hatua Nyingine  Afisa Elimu Huyo Amewashauri wadau wa Elimu  Pamoja na Wananchi  Mkoani Njombe  Kutoa Ushirikiano  Wa Kutosha na  Kutokuwakatisha   Morali Walimu Wapya  waliopangiwa  ambao wanatarajia Kuanza   Kutoa Elimu Katika Mkoa wa Njombe.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo