MAUAJI YA WATU YAWA TISHIO MKOANI NJOMBE

Na Edina Ngavatula Njombe.
 Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limethibitisha Kutokea Kwa Kifo cha Costatino  Herman Mayemba  Mwenye Umri Wa Miaka 62  Mkazi  Wa  Kijiji Cha Ngalanga Kata ya Uwemba Wilayani Njombe

Kwa Mujibu wa Taarifa Iliyosainiwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgency Ngonyani (pichani) Imeeleza Kuwa Tukio Hilo Limetokea  Machi 31 Mwaka Huu  Majira Ya Saa 1:00 Jioni Huko Katika Kijiji cha Ngalanga Baada ya Mtu/Watu Wasiojulikana Kuingia Ndani Ya Nyumba Yake na Kumuuwa Kwa Kumkata na Kitu Chenye Ncha Kali Sehemu za Kichwani.

Taarifa Hiyo Imefafanua Kuwa Marehemu Alikutwa Chumbani Kwake Akiwa Ameuawa Wakati Familia Yake Ikiwa Shambani.

Aidha Taarifa Hiyo Imesema Kuwa Hakuna Mtu/Watu Wanaoshikiliwa na Jeshi Hilo Kwa Kuhusika na Tukio Hilo na Kwamba Jeshi la Polisi Linaendelea na Uchunguzi wa
Mauaji Hayo.

Pamoja na Mambo Mengine Wito Umetolewa Kwa Watu Wenye Taarifa ya Waliohusika na Tukio Hilo Ili Waweze Kukamatwa na Kufikishwa Kwenye Vyombo Vya Sheria.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo