Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Mama Maria Nyerere Nishani ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungnao Daraja nne.
Mama
Fatma Karume akipokea Nishani ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya
Muungano(Order) kwa niaba ya Marehemu Abeid Aman Karume Rais wa Zanzibar
na mwenyekiti wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Mama Fatma Karume nishani ya
kumbukumbu ya Miaka 50 ya Muungano Daraja Nne wakati wa hafla ya
kutunuku nishani na tuzo za miaka 50 Muungano zilizofanyika katika
ukumbi wa mikutano ikulu jijini Dar es Salaam jana usiku.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Rais mstaafu wa Awamu ya tatu
Mh.Benjamin William Mkapa Nishani ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya
Muungano(Order) wakati wa sherehe ya kutunuku nishani na tuzo
iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano ikulu jijini Dar es Salaam jana
usiku.(picha na Freddy Maro)
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Nishani ya Kumbukumbu ya
miaka 50 ya Muungano Daraja la Kwanza Waziri Mkuu mstaafu ambaye pia
alikuwa Mwenyekiti Tume ya kurekebisha Katiba Mhe. JajiJoseph Sinde
Warioba wakati wa Sherehe hizo zilizofanyika katika ukumbi wa mikutano
ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete usiku wa kuamkia leo ametunuku nishani
na Tuzo kwa viongozi mbalimbali wa kitaifa na watumishi wa umma wapatao
86 waliotoa mchango wao katika kuulinda na kuudumisha muungano wa
Tanganyika na Zanzibar uliodumu kwa miaka Hamsini 50.
Picha zote na Freddy Maro