Wakati
wa Sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tarehe 26 Aprili 1964,
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa
Zanzibar Abeid Amaan Karume ambao sasa wote ni marehemu, walipanda
katika shimo moja miembe
miwili mmoja kutoka Zanzibar na mwingine kutoka Tanganyika. Miembe hiyo
imekuwa na kustawi pamoja na kufanya shina moja 'through grafting' .Leo
hii mti huo wa
mwembe umestawi vyema katika bustani ya Ikulu, Dar es Salaam, kama
unavyoonekana leo Aprili 26, 2014 ambayo ni Siku ya miaka 50 ya
Muungano.
MWEMBE ULIOPANDWA NA NYERERE NA KARUME KATIKA IKULU YA DAR ES SALAAM HUU HAPA
By
Edmo Online
at
Saturday, April 26, 2014
