MWISHO WA KUPIGA KURA KILI MUSIC AWARDS 2014 NI APRILI 30 MWEZI HUU

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe akiongea na waandishi wa Habari muda mfupi juu ya mchakato mzima wa tuzo za Kili Music Awards 2013- 2014, ndani ya Jengo la kampuni hiyo lililopo Masaki jijini Dar es Salaam.
Msemaji kutoka kampuni ya kuratibu hesabu na Utawala ya Aubitax Staraton Makundi naye akielezea namna kampuni yake inavyoratibu mchakato wa tuzo hizo.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini mchakato huo.

KAMPUNI Bia ya TBL inayozalisha kinywaji cha Kilimanjaro, leo imeweka wazi juu ya mwenendo wa shindano lake la Kili Music Awards ambalo linaendelea kwa sasa nchini kwa kuwapa fursa watanzania kuwapigia kura wasanii wa Muziki nchini katika vipengele vya tuzo hizo.

Meneja wa Kinywaji hicho, George Kavishe amesema kwamba baada ya Watanzania kupendekeza wasanii kwa mujibu wa vigezo vya BASATA na Academy,kupigia kura wateule kwenye vipengele hivyo sasa watanzania wanatakiwa kupiga kura za mwisho ili kukamilisha asilimia 70 zinazotarajiwa kupatika kutoka kwa wapenzi wa muziki huo.

Aidha Kavishe aliweka wazi kwamba mchakato wa upigaji kura unatarajiwa kufungwa itakapofikia tarehe 30 mwezi huu na baada ya hapo wasanii na mashabiki wao watakutana kwa pamoja tena tarehe 3 mwezi wa tano mwaka huu, ambapo itakuwa ndiyo siku rasmi ya washindi kukabidhiwa tuzo zao.

“Naomba watazania wapige kura kwa wingi maana hii ndiyo wiki ya mwisho ya kumpatia kura msanii uanayempenda, maana ukishindwa kufanya hivyo ndani ya wiki hii utakuwa umepoteza haki yako ya msingi kwani zoezi hili linatarajiwa kufungwa mara moja itakapofika tarehe 30 mwezi huu,” alisema Kavishe.

(Habari/Picha: Musa Mateja/GPL.)


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo